Joshua 12:1-6

Orodha Ya Wafalme Walioshindwa

1 aHawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:

2 bSihoni mfalme wa Waamori,

ambaye alitawala huko Heshboni. Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi.

3

cPia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi
Yaani Bahari ya Galilaya.
hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi
Yaani Bahari Mfu.
), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga.

4 fNayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani,

aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.

5

gNaye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.

6 hMusa, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Musa mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.

Copyright information for SwhKC